India yarejeshwa katika Olimpiki.

Image caption Mwakilishi wa India Sochi

Viongozi wa Kamati ya Olimpiki duniani wameirejeshea India kiti chake katika kamati ya olimpiki duniani (IOC)baada ya kutimuliwa yapata mwaka mmoja uliopita.

India ilipigwa marufuku kutokana na shtuma kuwa ilikuwa imeingilia kati uchaguzi wa kitaifa wa kamati ya olimpiki nchini humo .

Kamati ya Olimpiki duniani iliagiza kufanyike mabadiliko ya katiba ya shirikisho la India mbali na kuruhusu uchaguzi huru na wa haki kufanyika.

Hata hivyo kurejeshwa kwa India haitakuwa afueni kwa wanariadha kutoka taifa hilo wanaoshiriki mashindano ya olimpiki ya msimu wa baridi huko Sochi Urusi chini ya bendera ya Kamati ya Olimpiki duniani wala sio ile ya India .