Uwanja wa Etihad kupanuliwa zaidi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Uwanja wa Etihad

Mradi wa kuongezeka idadi ya mashabiki katika uwanja wa Manchester City kutoka mashabiki elfu arubaini na nane hadi elfu sitini na mbili umeidhinishwa.

Klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Premier nchini England, itajenga maeneo zaidi ya mashabiki katika uwanja huo.

Mradi huu utajumuisha ujenzi wa maeneo mawili yatakayokuwa na mashambiki elfu nane zaidi.

Ujenzi huo utaifanya uwanja huo wa Etihad kuwa wa pili kwa ukumbwa nchini Uingereza baada ya uwanja wa Manchester United wa Old Trafford.

Madiwani wa baraza la jiji la Manchester, waliidhinisha mradi huo, ambao unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Manchester City ilihamia uwanja huo mwaka wa 2003.

Awali Uwanja huo ulikuwa na idadi ya kuchukua mashabiki elfu thelathini na nane, wakati ilipojengwa mwaka wa 2002, kwa matumizi ya michezo ya Jumuiya ya madola.