Azam ya TZ yaondolewa michuano ya Afrika

Image caption Azam ilichapwa mabao 2-1na Feroviario de beira ya Msumbiji

Ilikuwa Wiki ya Majonzi kwa mashabiki wa soka nchini Tanzania baada ya wawakilishi wao kwenye Michuano ya Soka kuwania Kombe la shirikisho barani Afrika Azam FC kutupwa nje ya michuano hiyo kufuatia Kichapo cha bao 2-0 dhidi ya Feroviario de Beira ya Msumbiji hapo jana Jumapili mjini Beira.

Kufuatia kichapo hicho cha ugenini Azam imeaga michuano hiyo kwa kichapo cha bao 2-1 kufuatia ushindi mwembamba wa bao 1-0 iliokuwa imeupata katika mechi ya awali mjini Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo Azam imeaga michuano hiyo na kuiacha Yanga ya Dar es Salaam kubeba bendera ya matumaini ya Watanzania kwenye Michuano ya kuwania Klabu Bingwa barani Afrika ambapo sasa inajiandaa kuikabili National Al Ahly ya Misri ambao ni Mabingwa watetezi baadae mwezi huu,baada ya kuitupa nje Comorozine ya Comoro kwa ushindi wa jumla wa bao 12-2.

Mechi hiyo ya Yanga dhidi ya Mabingwa hao wa Afrika Al Ahly ,tayari imeshaanza kuwa gumzo kubwa jijini Dar es Salaam na Tanzania nzima kwa ujumla hasa kutokana na historia uimara wa Timu za Misri hususan kwenye Michuano ya soka barani Afrika,ambapo kwa miaka Mingi Timu kutoka Misri zimekuwa zikizitesa klabu za Tanzanzia hususan Simba na Yanga ingawa Timu ya Simba mwaka 2003 ilifanikiwa kuivua Ubingwa Zamalek na kuweza kutinga hatua ya nane bora katika kuwania Kombe la Ligi ya Mabingwa barani Afrika