UN kuzindua dhulma za Korea Kaskazini

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Banki Moon

Umoja wa mataifa, unatarajiwa kuzindua ripoti maalum inayosimulia dhulma za haki za binadamu zinazotekelezwa Korea Kaskazini.

Wanaharakati za haki za kibinadamu,waliofanya uchunguzi huo kwa kipindi cha mwaka mzima wamesema kuwa wamegundua dhulma na ukatili unaotekelezwa na serikali ya korea kaskazini dhidi ya wanainchi wake.

Watafiti wanasema kuwa Korea Kaskazini inawatendea unyama raiya wake na kuwa unakiuka maadili ya jamii ya kimataifa.

Mwanamke mmoja mfungwa aliyehojiwa, anasema kuwa alilazimishwa kumua mwanawe kwa kumtumbukiza ndani ya maji .

Serikali vilevile ilipatikana na hatia ya kuwafunga jela watoto tangu kuzaliwa wengi wakinyimwa chakula .

Ripoti hii inatarajiwa kutoa ushahidi wa kwanza na muhimu kuwa serikali ya kiimla ya nchi hiyo inatumia mbinu za kibepari kupunguza idadai ya watoto wanaozaliwa.