Euro 2016: Baadhi zapangwa kundi la kifo

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwonekano wa kiwanja cha Aliianz Riviera mjini Nice nchini Ufaransa

Timu ya taifa ya Scotland na Jamuhuri ya Ireland zimepangwa katika moja ya makundi magumu katika michuano ya kufuzu kwa ajili ya fainali za mataifa barani ulaya mwaka 2016.

Katika kundi lao nchi nyingine zinazoungana nazo ni Ujerumani, Poland, Georgia na Gibraltar.

Uingereza itakutana na Switzerland, Slovenia,Estonia,Lithuania na San Marino, huku Wales ikiwa kundi moja na Bosnia-Hercegovina,Belgium,Israel,Cyprus na Andorra.

Ireland kaskazini iko kundi F pamoja na Ugiriki,Hungary, Romania, Finland na Faroe Islands.

Michuano ya Euro mwaka 2016 itahodhiwa na Ufaransa, ambayo moja kwa moja imefuzu, michuano ambayo itahusisha mataifa 24, kutoka idadi ya nchi 16 katika michuano iliyopita.