Mourinho: Alalama kurekodiwa kwa siri

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Jose Mourinho kocha wa Chelsea

Kocha wa timu ya Chelsea ya England, Jose Mourinho ameshutumu tabia ya kurekodi kwa siri mazungumzo yake kuhusu wachezaji wa timu hiyo.

Mourinho amesema lilikuwa jambo la aibu kuona kwamba mazungumzo binafsi kuhusu wachezaji wa timu yake, yanawekwa hadharani na kampuni moja ya televisheni nchini Ufaransa.

Mourinho amesema alikuwa anatania alipokuwa akilalamika kuwa Chelsea inakosa wachezaji wa nafasi ya ushambuliaji na alimtania Eto'o kuhusu umri wake.

"Yalikuwa mazungumzo ya utani na mtu ambaye hahusiki na masuala ya ulimwengu wa soka," amesema Mourinho.

"Ni fedheha kwa mtu kurekodi mazungumzo binafsi."