Lewis Hamilton asema Red Bull ni moto!

Haki miliki ya picha PA
Image caption Bingwa wa dunia Lewis Hamilton.

Dereva wa timu ya Mercedes katika mbio za Langalanga Lewis Hamilton amesema kuwa anatarajia madereva wa timu ya Red Bull kuzua upinzani mkali katika mashindano ya mwaka huu licha ya kuandikisha matokeo duni katika mazoezi ya kabla ya msimu.

Timu ya Red Bull imekumbwa na tatizo baada ya tatizo katika kipindi cha mazoezi majira ya baridi lakini Hamilton amesema; " Inaelekea wana magari maridadi zaidi, na kwa kawaida, kadri gari linavyoonekana kuwa maridadi zaidi ndivyo lina uwezo wa kwenda kwa kasi zaidi.''

"Kwa hiyo nina uhakika wana gari lenye kasi kubwa kabisa. Na punde tu watakapomaliza kurekebisha matatizo ya kimitambo, itakuwa vigumu kuwashinda."

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Dereva mashuhuri Lewis Hamilton wa Uingereza akifanya vitu vyake katika Mercides GP.

Mazoezi ya kabla ya msimu yalikamilika siku ya Jumapili nchini Bahrain huku Hamilton, mwenye umri wa miaka 29, akiasajili muda wa kasi zaidi.

Mwaka 2008 bingwa huyo wa dunia alisema kuwa alikuwa na matumaini timu ya Mercedes ndio itakayokuwa katika nafasi nzuri ya kunyakuwa ubingwa msimu huu, ambao umeshuhudia mageuzi makubwa ya kisheria, madereva wakiruhusiwa kutumia wakiruhusiwa kutumia magari yenye engine zenye uwezo mkubwa wa ''turbo hybrid''

" Najua timu yangu ni dhabiti na hivyo nina matumaini tutaweza kupambana nao (Red Bull)," Hamilton amesema.