Historia itajirudia Ujerumani 'Wenger

Haki miliki ya picha y
Image caption Arsenal vs Bayern

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger anatarajia historia itajirudia huko Ujerumani timu yake ilaze Bayern Munich katika mechi ya mkondo wa pili wa ligi ya mabingwa barani Uropa usiku wa leo.

Bayern, inaikaribisha Arsenal katika uwanja wa Allianz Arena, ikiazimia kuwa timu ya kwanza kuwahi kuhifadhi kombe hilo .

Wajerumani hao walishinda mkondo wa kwanza mabao 2-0.

Wenger anakumbuka vyema matokeo ya mwaka uliopita Arsenal ilipobanduliwa nje ya mchuano huu kutokana na sheria ya bao la Ugenini.

Bayern ilishinda mabao 3-1 katika uwanja wa Emirati lakini vijana wa wenger wakaitamausha bayern mabao 2-0 huko Munich.

Bayern inajivunia rekodi ya kutoshindwa katika mechi 16 katika ligi ya nyumbani ya Bundesliga na zaidi ya alama 20 zaidi ya washindi wapili.

Gonga Gonga

Bayern Munich ilikamilisha pasi 863 ikilinganishwa na 222 za Arsenal 222 katika mkondo wa kwanza uliochezwa February 19.

Hiyo iliwakilisha 78.8% ya umiliki wa mpira katika kipindi cha pili.

Arsena iliwahi mipira takriban asilimia 12% pekee ya kipindi hicho.

Aidha Mabingwa hao watetezi walitwaa mataji mawili ya ligi ya nyumbani mbali na kuibuka mabingwa barani Uropa hayo yote katika msururu wa mechi 49 bila ya kushindwa . Bayern haijashindwa tangu Oktoba mwaka wa 2012.

Licha ya rekodi hiyo Wenger anasisitiza kuwa kikosi chake kinatamaa ya kufanya vyema na kuwa historia inadhihirisha wazi kuwa Arsenal inaweza kushinda na inaari ya kufanya hivyo katika mechi ya leo usiku.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Arsenal vs Bayern

Arsenali imewahikushinda mechi Tatu kati ya Tano ilizocheza dhidi ya Bayern nyumbani kwao na ikatoka sare katika mechi mbili zilizosalia.

Kocha huyo mfaransa alinukuliwa akisema kuwa refarii ndiye aliyesababisha mechi ya mkondo wa kwanza kumwendea segemnege baada ya kumwonesha kipa Wojciech Szczesny kadi nyekundu mapema katika kipindi cha kwanza . Kocha wa Bayern Pep Guardiola anakila sababu ya kumakinika baada ya Toni Kroos na Thomas Muller,kufunga mabao hayo muhimu lakini akafaidi bahati baada ya Mesut Ozil kukosa kufunga penalti katika mechi hiyo.