Tanzania nje ya mchuano wa Raga Bamburi

Image caption Timu ya Kenya ya raga ya Tusker XV;s

Timu sita pekee ndizo zitakazoshiriki mchuano wa raga ya wachezaji 15 kila upande wa Bamburi Super Series ambao hushirikisha timu kutoka Kenya Tanzania na Uganda.

Kulingana na mwenyekiti wa shirikisho la raga nchini Kenya Mwangi Muthee kupunguzwa kwa idadi ya timu kutoka timu nane hadi sita imetokana na haja ya timu shiriki kuimarisha mazoezi kuafikiana na mabadiliko ya mfumo wa mazoezi ambao sasa inazingatia utafiti wa kisayanzi .

Aidha Muthee alisema kuwa idadi hiyo imepunguzwa ilikuchochea ushindanibaina ya timu zinazoshiriki .

Katika mfumo huu mpya Kenya itatoa timu nne huku Uganda ikiwakilishwa na timu mbili .

Tanzania ambayo kawaida ilikuwa inawkilishwa na timu ya Twiga imeachwa nje ya ratiba ya mwaka huu .

Uganda itawakilishwa na Ruwenzori na Victoria.

Timu zitakazoiwakilisha Kenya zitakuwa Mabingwa watetezi Ndovu, Chui , Kifaru na Papa.

Kifaru itajumuisha wachezaji mseto kutoka vyuo vikuu nchini Kenya .

Mchuano utaanzia huko Uganda tarehe 26 April na kumalizika tarehe 7 Juni baada ya kuzuru miji mitano.

Mechi zote za kwanza zitaandaliwa mjini Kampala Uganda.

Mechi za raundi ya pili zimeratibiwa kufanyika magharibi mwa Kenya katika mji wa Kakamega .

Nakuru nayo itaanda mkondo wa nne wa mchuano wa mwak huu katika mfumo huu mpya wa ''super sato'' ambao unajumuisha mechi zote katika eneo moja kwa minajili ya kuvutia mashabiki wengi zaidi .

Mechi za nusu fainali zitaandaliwa katika uwanja mpya wa Kenyatta ulioo mjini Machakos Kenya huku fainali ikiratibiwa kufanyika katika uwanja wa taifa wa RFUEA mjini Nairobi.

Mshindi atatuzwa shilingi milioni moja pesa za kenya sawa na dola elfu kumi na moja pesa za marekani.

Kampuni ya saruji ya Bamburi ilitoa udhamini wa shilingi milioni 20 za Kenya US $238,095 kufadhili mchuano wa mwaka huu.

Kenya inatumia mashindano haya kujiandaa kwa mechi za kufuzu kwa kombe la dunia zitakazoandaliwa nhini Madagascar ,kutokana na hilo mwenyekiti shirikisho la raga nchini Kenya ametangaza kuwa kikosi cha timu ya Western Province ya Afrika Kusini itazuru Kenya mapema mwezi juni kwa mechi ya kirafiki ya kimataifa .

Timu ya Kenya Tusker XV's iliweka historia iliposhinda mechi yake ya ufunguzi dhidi ya Eastern Province Kings alama 17-10 .

Timu hizo zilikuwa zimetoshana nguvu kufikia muda wa mapumziko alama 5-5 katika uwanja wa City Park, Cape Town .

Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa timu ya Kenya kushiriki mchuano huo wa Vodacom Cup .