Malawi nje ya michuano ya Afrika 2015

Timu ya taifa ya soka ya Malawi, imelazimika kujiondoa kutoka katika mechi za kufuzu kwa kombe la taifa bingwa Afrika nchini Morocco mwaka 2015 kutokana na kukosa ufadhili.

Uamuzi huo ulifikiwa baada ya serikali kusema kuwa haina pesa za kutosha kwa timu hiyo kucheza katika michuano ya kufuzu kwa kombe la laifa bingwa Afrika mwaka 2015 pamoja na kombe la vijana.

"hatuna budi ila kujiondoa kutoka mchuano mmoja na utakuwa mchuano wa kombe la taifa bingwa Afrika kwa sababu serikali imetushauri kufanya chaguo moja, '' alisema mkuu wa shiriki sho la soka la Malawi, Walter Nyamilandu.

"kwa hivyo tumeamua kushiriki mchuano wa vijana walio chini ya umri wa miaka 20 kwa ajili ya maendeleo, na pia athari za kujiondoa katika michuano hiyo ingekuwa mbaya kwa sababu tumeshaelezea kuwa tuko tayari kushiriki. ''

Bila shaka ni pigo kubwa kwa timu yetu, iliyorejea kutoka mechi kwa mara ya kwanza katika miezi sita wakicheza mechi ya kirafiki na Zimbabwe iliyoshindwa kwa mabao 4-1.

Mechi hiyo, ilinuiwa kuanza maandalizi ya Malawi katika kushiriki katika mechi za kufuzu za kombe la taifa bingwa Afrika.

Septemba mwaka jana, serikali ya Malawi, ilishauri shirikisho la soka Malawi kutocheza mechi ya kufuzu kw akombe hilo dhidi ya Nigeria kwani pesa ilizotengewa zilikuwa zimekwisha.

Lakini shirikisho hilo liliendelea na mipango yake na kulazimisha serikali kuipa pesa za ziada.