Barcelona yatamba, Man City yabanduliwa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Manchester City baada ya mechi yao na Barcelona

Dani Alves alifunga bao dakika za mwisho ya mechi yao na kuipa Barcelona ushindi dhidi ya Manchester City na kufuzu kwa robo fainali ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya.

Manchester ambayo ilinyukwa magoli mawili kwa bila katika mechi ya raundi ya kwanza, ilipoteza nafasi nyingi wakati wa mechi hiyo nzuri zaidi ikiwa ni mkwaju wa Samir Nasri uliookolewa na kipa wa Barcelona Victor Valdes.

Lionel Messi alikamilisha pasi ya Cesc Fabregas kati kati mwa kipindi cha pili kabla ya Pablo Zabaleta kuonyeshwa kadi nyekundu.

Baada ya kushinda kombe la Ligi mwishoni mwa Juma lililopita na kupoteza mechi ya robo fainali ya kuwania kombe la FA dhidi ya Wigan, vijana hao wa Manuel Pelegrini sasa wamesalia la katika kinyanganyiro cha kuwania kombe la Ligi Kuu ya Premier na kwa sasa inashikilia nafasi ya nne ikiwa alama tisa nyuma ya vinara wa sasa Cheslea lakini ingali na mechi tatu mkononi.

Manchester City sasa itasubiri kwa hamu kuu habari kuhusu jeraha lililomlazimisha Sergio Aguero, ambaye tayari amekosa mechi kadhaa msimu huu, kuondolewa baada ya kipindi cha kwanza.

Hata hivyo City waligadhabisha na uamuzi wa refa wa mechi hiyo kutoka Ufaransa Stephan Lannoy, wa kupuuza kile kilichoonekana kuwa penalti ya wazi baada ya Gerard Pique kumfanyia madhambi Zabaleta ambaye alipewa kadi nyekundu baada ya kuonyesha kadi ya njano ya pili.

Machester City ilipata bao lake la kuvutia machozi kupitia kwa nyota wake Jeleon Lescott.

Barcelona imefuzu kwa robo fainali kwa jumla ya magoli manne kwa m