Van Persie kusaini mkataba mpya

Haki miliki ya picha PA
Image caption United Robin van Persie

Mshambulizi wa Manchester United Robin van Persie amesema kuwa yuko tayari kuongeza muda wa mkataba wake.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka thelathini amekuwa akihusishwa na madai ya kutaka kukihama klabu hiyo kwa kuwa hana uhusiano mwema na kocha wa David Moyes na kumekuwa na fununu kuwa huenda akaondoka mwishoni mwa wa msimu huu.

Lakini mchezaji huyo kutoka Uholanzi amesema kuwa anaridhika kucheza chini ya Moyes.

Katika michuano ya kuwania kombe la Uropa, Tottenham itakuwa na kibarua kigumu kufunga zaidi ya magoli mawili wakati wa mechi yake ya raundi ya pili, baada ya kufungwa magoli matatu kwa moja na Benfica, katika uwanja wa White Hart Lane.

Image caption Emmanuel Adebayor

Mchezaji wa zamani wa Bolton Rodrigo aliifungia benfica bao lake la kwanza kabla ya Luisao kuongeza magoli mawili katika mechi hiyo.

Emmanuel adebayor alipoteza nafasi nyingi za kufunga.

Tottenham ilipata bao lake la kuvutia machozi kupitia kwa nyota wake Christian Eriksen.

Benfica, ambayo ilishindwa na Chelsea kwa magoli 2-1 to katika fainali ya mwaka uliopita itakuwa na nafasi nzuri ya kufuzu kwa raundi ijayo wakati itakapocheza nyumbani.