Steven Gerrard ammwagia sifa Rodgers

Haki miliki ya picha PA
Image caption Kocha wa Timu ya Liverpool, Brendan Rodgers

Nahodha wa timu ya Liverpool Steven Gerrard amesema kuwa Kocha wa Timu hiyo Brendan Rodgers ni Kocha bora ambaye amewahi kufanya nae kazi.

Rodgers raia wa Ireland kaskazini alijiunga na Liverpool mwaka 2012.

Gerrard amemmwagia sifa Rodgers amekuwa akifanya mabadiliko mbalimbali katika kuboresha timu yake na wachezaji hali ambayo Gerrard ameeleza humfanya mchezaji kuwa katika hali ya kujiamini na matumaini.

Nahodha huyo wa England pia ametoa wito kwa mmiliki wa timu ya Liverpool kumtunuku Rodgers na mkataba mwingine wa muda mrefu, baada ya mkataba huu ambao unamalizika mwishoni mwa msimu ujao.

Gerrard amesema wanafurahia mno uwepo wake ndani ya Liverpool na kuwa anastahili kuwa katika nafasi aliyonayo sasa na amekuwa akionesha jitihada kila siku.

Timu ya Liverpool imeshika nafasi ya pili katika michuano ya Ligi kuu, ikiwa na alama nne nyuma ya Chelsea.

Gerrard hakuwahi kushinda michuano ya ligi kuu, akiwa na Liverpool, isipokuwa kuibuka washindi wa pili mwaka 2001-2002 wakati ambapo Kocha wa timu hiyo alikua Gerard Houllier pia mwaka 2008-09 chini ya Rafael Benitez.

Hodgson ni mmoja wa Makocha saba ambao wamefanya kazi na Gerrard kimataifa, sambamba na Fabio Capello,Steve-Goran Eriksson, Kevin Keegan halikadhalika Stuart Pearce na Peter Taylor.