Real Madrid 9-2 Shalke 04

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ronaldo

Mchezaji bora duniani mwaka huu Cristiano Ronaldo alifunga mabao mawili na kuisadia timu yake ya Real Madrid ya Uhispania kufuzu kwa hatua ya timu nane bora za ligi kuu ya mabingwa

Uropa baada ya kuinyuka Schalke 04 kutoka Ujerumani mabao 3-1 katika mechi ya mkondo wa pili iliyochezwa katika uwanja wao wa nyumbani ,Bernabu.

Ronaldo alifungua kichapo hicho kwa kutinga wavuni pasi safi kutoka kwa Gareth Bale katika eneo la lango.

Schalke ilisawazisha dakika kumi baadaye beki Tim Hoogland alipofunga mpira uliokuwa umetemwa na nahodha wa wenyeji wao Iker Casillas.

Wajerumani hao walihimili wimbi baada ya wimbi la mashambulizi kutoka kwa Madrid na juhudi zao zilitumbukia nyongo kukanko dakika ya 74 ya kipindi cha pili ,Ronaldo alipofunga bao lake la 41 msimu

huu .

Dakika moja baadaye Alvaro Morata aliiadhibu safu ya ulinzi ya Shalke kwa kuzembea alipofunga bao la tisa la Madrid na hivyo kudhibitisha hofu ya kocha wa Schalke Jens Keller kuwa hakukuwa na

matumaini yeyote ya timu hiyo ya Ujerumani kusonga mbele baada ya kutandikwa mabao 6-1 katika mkondo wa kwanza huko Ujerumani.

Madrid inasonga mbele ikiwa na jumla ya mabao 9-2 dhidi ya Shalke 04 ya Ujerumani.

Wawakilishi wengine wa Ujerumani katika ligi ya mwaka huu ni mabingwa watetezi Bayern Munich na Borussia Dortmund.

Image caption Jesse Kiungo wa Real Madrid aliyejeruhiwa

Wakati huohuo kiungo cha Real Madrid Jese hatoshiriki mechi yeyote msimu huu baada ya kujeruhiwa vibaya katika mechi hiyo dhidi ya Shalke 04.

Jesse mwenye umri wa miaka 21 alianguka vibaya baada ya makabiliano na beki wa Schalke Sead Kolasinac na akalazimika kubebwa kwenye machela daktari akisema ni jereha la goti.

Kocha wa klabu hicho tajiri duniani Carlo Ancelotti amedhibitisha kuwa Jesse ameumia kiasi cha kuwa amefunga msimu na kuwa klabu hicho kitamsaidia katika matibabu ya jeraha hilo la

goti hadi atakaporejea msimu ujao.

Jesse ameichezea Madrid katika mechi 31 na kuifungia mabao 8, la kwanza likiwa bao dhidi ya mahasimu wao wa jadi Barcelona mwaka uliopita.

Kutokana na ushindi huo mkubwa Madrid sasa inajiunga na Barcelona na Athletico Madrid katika droo ya hatua ijayo ya robo fainali inayotarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa.

Real vilevile inatarajia kuendeleza msururu wa matokeo mema katika ligi yao ya nyumbani La liga ambapo imeratibiwa kukwaruzana na watani wao wa jadi Barcelona siku ya Jumapili katika mechi

inayotizamiwa na mashabiki wengi zaidi duniani ya el -Classico.