Man United wamenyana na Man City

Haki miliki ya picha Getty
Image caption David moyes

Aliyekuwa mchezaji maarufu wa mabingwa wa ligi kuu Manchester united Charlton amesema kuwa mabingwa hao wanaotarajiwa kupambana na timu ya Manchester city siku ya jumanne Usiku, wamecheza vibaya sana msimu huu.

Hata hivyo Charlton mwenye umri wa miaka 76 amenukuliwa akisema kuwa hapakuwa na haja ya kubadili kila kitu kwani ana uhakika kuwa David Moyes anatosha kama kocha.

Timu ya united kwa sasa ipo katika nafasi ya saba katika ligi hiyo ikiwa imesalia na mechi nane tu.

Wakati huo huo united ina alama kumi na moja nyuma ya Arsenal iliyo ya nne na alama 18 nyuma ya viongozi Chelsea, ingawa walifuzu robo fainali ya ligi ya mabingwa.

Ikiwa wataishinda timu ya Manchster City huenda nafasi yake katika orodha ya ligi ikapanda juu ijapokuwa huenda ikawa hawatakuwa katika nafasi nne za kwanza msimu huu.

Mkufunzi wa united David moyes ameonyesha imani kuwa watarejea katika upeo wa mbele huku akisema kuwa mpira ni mzunguko na haitowachukua muda murefu kabla yao wao kurudi katika nafasi za uongozi wa ligi huku akiongeza kuwa ingawa kwa sasa United iko nyuma ya klabu ya Manchester city wanakusudia kubadili hayo kwa kuimarisha mchezo wao.

Nani ataibuka mshindi? toa utabiri wako hapa: https://www.facebook.com/pages/BBC-Swahili/160894643929209?ref=hl