Phelps kuogelea tena

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Michael Phelps kurejea katika mashindano ya uogeleaji

Bingwa wa dunia katika mashindano ya uogeleaji, Michael Phelps anapania kurejea tena katika ulingo wa uogeleaji hivi karibuni.

Mkufunzi wake Bob Bowman anasema mwogeleaji huyo angali ana muda mrefu wa kupiga mbizi majini kabla ya kustaafu.

Mmarekani huyo mwenye umri wa miaka 28 ambaye ameshinda medali 22 ya Olimpiki, anatarajiwa kushiriki mashindano ya Arizona mwishoni mwa mwezi huu wa Aprili.

Phelps alistaafu baada ya kushinda medali yake ya 18 ya dhahabu ya olimpiki huko London.

Phelps anayefahamika kama The Baltimore Bullet ndiye anayeshikilia rekodi ya kuwa mwanaspoti aliyewahi kushinda nishani nyingi zaidi za dhahabu katika mashindano moja alipotwaa ubingwa katika mashindano 8 ya uogeleaji huko Beijing mwaka wa 2008.

Image caption Michael Phelps kurejea katika mashindano ya uogeleaji

Bowman amesema kuwa Phelps atashiriki katika mashindano tatu ya uogeleaji ile ya mita 100 mtindo wa butterfly mita 50m na 100m mtindo wa freestyle katika mashindano hayo yatakayofanyika tarehe 24 mwezi huu.

Kocha Bob Bowman alikuwa ameiambia BBC mwaka uliopita kuwa Phelps anapania kushinda medali zaidi za katika mashindano ya olimpiki ya Rio de Janeiro Brazil mwaka wa 2016.

Phelps alirejea mazoezini mwaka uliopita na sasa amekamilisha muda wa makataa ya miezi 6 ya uchunguzi wa utumizi wa madawa na sasa yu tayari kwa mashindano.

Muogeleaji huyo Stadi sasa atapimana nguvu na waogeleaji nyota Ryan Lochte na Katie Ledecky katika mashindano hayo ya Mesa.

Phelps si mwogelaji wa kwanza kurejea mashindanoni baada ya kustaafu.

Mwaka wa 2012 muogeleaji Ian Thorpe, kutoka Australia alijaribu kurejea mashindanoni lakini akashindwa.