Mourinho achukizwa matokeo ya droo

Image caption Meneja wa Chelsea Jose Mourinho

Meneja wa timu ya Chelsea ya England, Jose Mourinho ameelezea kipindi cha mchezo kati ya timu yake na Norwich katika uwanja wake wa Stamford Bridge kama "kupoteza muda" katika mchezo huo uliomalizika kwa 0-0.

Amewashutumu wachezaji wake kwa mchezo wa "polepole" na "uvivu" katika mchezo kabla ya kipindi cha kwanza, lakini katika kipindi cha pili ilikuwa "tofauti kabisa".

Japokuwa Chelsea ilikosa nafasi ya kupaa kileleni mwa ligi kwa kuambulia pointi moja badala ya tatu ilizohitaji katika mchezo wake dhidi ya Norwich, lakini wako nafasi ya tatu na moja kwa moja kujihakikishia kucheza mashindano ya ligi ya mabingwa Ulaya, UEFA.

Mpaka sasa Manchester City wanaongoza kwa pointi 80 sawa na Liverpool iliyoko nafasi ya pili zikitofautiana kwa wingi wa magoli ya kufunga. Manchester City ina magoli 59 na Liverpool ina magoli 50 baada ya zote kucheza mechi 36.

Vinara hao wamebakiza mechi mbili mbili kukamilisha ligi kuu ya England msimu