Mchezaji wa NFL ajitangaza kuwa shoga

Haki miliki ya picha Getty

Mchezaji mmoja wa timu ya ligi ya soka ya Marekani, National Footbal League ,Michael Sam amekuwa mchezaji wa kwanza kutangaza wazi kwamba yeye ni shoga katika mchezo huo.

Sam alikuwa ameteuliwa na timu ya Saint Louis Rams katika siku ya mwisho ya usakaji wa vipaji katika mchezo huo ulio maarufu zaidi nchini marekani.

Hatua hiyo ya Michael Sam kutangaza jinsia yake mnamo mwezi february baada ya kukamilisha masomo yake ya mchezo huo katika chuo cha Missouri ilipongezwa ,huku rais Obama akiwa miongoni mwa watu waliotoa pongezi zao.

Baadhi ya wachambuzi wa michezo walikuwa wamebashiri kwamba baadhi ya timu huenda zikajitenga na umaarufu unaomzunguka mchezaji huyo.