Mechi ya kupasha joto uwanja Brazil

Haki miliki ya picha not found
Image caption maandalizi ya kombe la dunia

Brazil mbioni kukamilisha ratiba ya maandalizi ya kombe la dunia.

Maandalizi ya kombe la dunia linalong'oa nanga 12 Juni huko Brazil yamepiga hatua baada ya mashabiki zaidi ya 30,000 kushuhudia mechi ya kwanza rasmi katika uwanja muhimu wa Sao Paulo.

Mechi ilihusu wenyeji Corinthians dhidi ya Figueirense, walio andika ushindi wa 1-0.

Mechi hiyo ilikuwa habari njema kwani maandalizi ya kombe hilo huko Brazil yamekumbwa na chelewa chelewa ikiandamana na misukosuko.

Mapema mwezi huu mamia ya waandamaji walijimwaga maeneo ya karibu na uwanja huo wakilalamikia fedha nyingi zilizotumiwa kwa maandilizi ya kombe hilo ilhali wao wanakumbwa na miundo mbinu duni ya usafiri huku gharama ya maisha iikipanda kila uchao.

Uwanja wa Sao Paolo ndio utakaofungua dimba hilo kwa mechi ya wenyeji Brazil dhidi ya Croatia na baadae kuwa mwenyeyeji wa mechi nyengine tano.