R.Madrid yashinda ubingwa wa ulaya

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wachezaji wa kilabu ya Real Madrid wabeba taji la kilabu bingwa barani Ulaya.

Timu ya Real Madrid imewacharaza mahasimu wao wa jadi katika ligi ya uhispania Atletico Madrid mabao 4 kwa moja katika fainal ya kombe la kilabu bingwa barani ulaya.

Ushindi huo ni wa kumi kwa timu ya Real Madrid.

Atletico Madrid ndio iliotangulia kucheka na wavu katika kipindi cha kwanza cha mchuano huo.

Atletico waliendelea kuongoza hadi katika mda wa majeraha ambapo Real Madrid ilikomboa na kuilazimu mechi hiyo kuchezwa katika mda wa ziada.

Na huku ikiwa imesalia dakika kumi ,Real Madrid ilipata mabao matatu kupitia wachezaji,Gareth Bale,Junior Marcelo na Christano Ronaldo.

Atletico Madrid haijawahi kushinda taji la ubingwa huo.