Kocha wa Atletico ajitetea kufungwa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Diego Costa kushoto na kocha wake Diego Simeone

Kocha Mkuu wa Atletico Madrid Diego Simeone amekiri kuwa alifanya makosa kumpanga Diego Costa katika mechi ya fainali baina ya timu hiyo na Real Madrid.

Real Madrid hapo jana iliibamiza Atletico Madrid kwa jumla ya magoli 4 - 1 na kunyakua kombe la Klabu Bingwa Barani Ulaya.

Costa alibadilishwa baada ya kuumia msuli wa paja ikiwa zimebaki dakika 9 mechi hiyo imalizike. Mshambuliaji huyo raia wa Hispania aliumia alipocheza mechi baina ya Atletico na Barcelona wiki moja iliyopita na ameweza kuifungia magoli 36 timu katika msimu huu.

"Hakuna mashaka kiwango alichoonyesha Diego uwanjani nina wajibu wangu nilifanya makosa lazima nikubali," Kocha Simeone alisema.

Mchezaji huyo ambaye ni mzaliwa wa Brazil alionekana kuwa chini ya kiwango na alibadilishwa na Adrian Lopez.

"Sitaki kupoteza muda tulicheza pungufu mchezaji mmoja", Kocha huyo alisema.