Clippers kugharimu dola billion 2

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Umiliki wa LA Clippers kumtoka Donald Sterling baada ya hatua kali kuchukuliwa dhidi yake kwa sababu ya kutoa matamshi dhidi ya wachezaji weusi.

Mkurugenzi wa zamani wa Microsoft, Steve Ballmer, amefikia makubaliano na timu mashuhuri ya mpira wa vikapu ya Los Angeles Clippers ya kuinunua timu hiyo kwa dola billion mbili.

Hata hivyo ununuzi huo unapingwa na mmiliki wa sasa Donald Sterling.

Haki miliki ya picha zloboglas
Image caption Mpira wa vikapu ni maarufu sana marekani. Na kwa sababu hushirikisha wachezaji wengi weusi matamshi ya Sterling yalihofiwa yangevuruga biashara ziinazotangazwa kupitia mchezo huo.

Sterling alitozwa faini ya £1.5m na pia amepigwa marufuku kuhusika kabisa na mchezo huo baada ya kashfa mliomkabili pale ilipoonekana kanda aliyorekodiwa akitoa matamshi ya ubaguzi wa rangi kuhusu wachezaji weusi wa mpira huo wa vikapu uliomaarufu sana Marekani.

Katika kushindania ununuzi huo ,Bw Ballmer aliwapiku wakinzani wake wawili akiwemo magwiji mahiri katika sekta ya vyombo vya habari akiwemo David Geffen na Oprah Winfrey.

Ballmer alistaafu kutoka Microsoft miezi mitatu iliyopita lakini bado ana kima kikubwa cha hisa katka kampuni hiyo zilizo na thamani ya zaidi ya dola billioni kumi na tatu.