Real yaadhibiwa kwa ubaguzi wa rangi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mabingwa wa Champions League shurti kutangaza vita dhidi ya ubaguzi wa rangi-UEFA

Shirika la kandanda la Europa, UEFA, limeiwekea vikwazo timu ya mpira ya Real Madrid kwa makosa ya mashabiki wao, waliotoa ishara na kejeli za ubaguzi wa rangi wakati wa moja ya mechi zake.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Je ni sawa Real Madrid kuadhibiwa na UEFA kwa sababu ya makosa yaliyofanywa na mashabiki wake?

Tukio hilo lilifanyika April wakati wa mechi ya nusu fainali kati ya mabingwa hao wa sasa wa kombe hilo la UEFA, na mahasimu wao,mabingwa wa zamani wa Bayern Munich.

Miongoni na adhabu walizopewa ni kufunga maeneo mawili ya uwanja wao wa Bernabeu wakati wa mechi yao itakayokuja ya UEFA na watapaswa kuweka mabango yaliyo na maandishi 'No to Racism' yaani 'Twakataa ubaguzi wa rangi!.