Oxfam yaanzisha Kombe la dunia mbadala

Haki miliki ya picha other
Image caption Nembo ya shirika la kutoa huduma za kibinadamu, Oxfam

Shirika la kutoa huduma za kibinadamu Oxfam limeendesha kile inachosema ni 'kombe la dunia mbadala' kuangazia pengo linalozidi kuwa kubwa kati ya maskini na matajiri katika mataifa yanayoshiriki kombe la dunia mwaka huu.

Ubelgiji imetangazwa mshindi kwa sababu si kuwa ina utajiri si haba bali pia ina mwanya mdogo zaidi kati ya raia wake matajiri na wenye kipato, ilhali wenyeji Brazil imefeli hata kufuzu raundi ya pili kwa jinsi pengo la umaskini na matajiri lilivyokumbwa miongoni mwa raia wake.

Mataifa mengineyo ya America kusini pia hayajafanya vizuri lakini yanasemekana kujitahidi, cha ajabu mataifa ya kiafrika yanayoshirki kombe la dunia hayajatajwa.