Hatma ya Rooney Brazil

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Wayne Rooney achezeshwe katika nafasi gani ?

Njama dhidi ya Wayne Rooney yaweza kuhatarisha matarajio yao katika kombe la dunia. Frank Lampard ameonya.

Uchunguzi wa nafasi yake Rooney katika timu hiyo ulizidi wakati Rooney alipocheza katika nafasi ambayo hakufaa, Uingereza iliposhindwa mabao 2-1 na Italia.

“Shughuli hizi nyingi kwa mchezaji mmoja hazitamsaidia yeyote,”alisema Lampard, mwenye umri wa miaka 35.

Raheem Sterling, aliyecheza katika nafasi ya kawaida ya Rooney, alisema kuwa kurudi kwao katika nafasi zao za kawaida kwaweza kuiletea uingereza mafanikio wakati timu hiyo itakapokutana na Uruguay siku ya Alhamisi.

Hata hivyo, Sterling, mwenye umri wa miaka 19 alisema kuwa itakua uamuzi wa mkufunzi wao kufanya hivo.

Alizidi kusema kuwa nafasi aliyoicheza Rooney katika mchuano uliopita, ndiyo iliyokua nafasi yake, naye Rooney akapewa nafasi hiyo, hivyo hakuweza kuitumia kikamilifu.

Image caption Kocha Hogson alaumiwa kwa kumchezesha Rooney asikofaa

Sterling alifanya utani kwa kusema kuwa alitarajia hatamwona mchezaji mwenza katika timu ya Liverpool, Luis Suarez uwanjani Arena de Sao Paulo wakati wa mechi yao.

Hata hivyo alisisitiza kuwa Uruguay ilikua na wachezaji wengine mashuhuri, zaidi na Suarez anayeuguza jeraha.

Mchezo mzuri ulioonyeshwa na Sterling katika mechi dhidi ya Italia umefanya ionekane kuwa Rooney aweza tena kunyimwa nafasi ya katikati ambayo ana mazoea nayo.

Lampard aliongeza kusema kuwa ni tukio la kutatanisha haswa katika mtazamo wa timu na tukio hilo laweza kugeuka na kuwa njama badala ya kuwa la kujadiliwa.

Lampard ambaye hakupata kupewa nafasi ya kucheza katika mechi yao ya kwanza alizidi kusema kuwa mchezaji mmoja akianza kulengwa mara kwa mara, timu nzima itaadhirika.

Rooney alifunga mabao 17 akiichezea Manchester United musimu uliopita lakini hajaifungia nchi yake bao lolote katika 9 ya michuano ya kombe la dunia ambayo ameshiriki.

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption Wayene Rooney achezeshwe katika nafasi gani ?

Mchezaji wa zamani wa Uingereza Allan Shearer, alisema heri Rooney aondolewe kikosini ikiwa hatapata kutumiwa katika nafasi ambayo aliizoea.

Hii ni licha ya pasi yake iliyoletea Daniel Sturridge kufunga bao la kusawazisha dhidi ya Italia.

Uamuzi wake Mkufunzi Roy Hodgson unakuja kabla ya mchuano muhimu kwani wakipoteza dhidi ya Uruguay, wataondolewa wakiwa katika hatua ya makundi kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1958.

Lampard alizidi kusema kuwa angependa wachezaji wa Uingereza kulenga kupata matokeo mazuri badala ya kucheza vizuri kisha kushindwa kama ilivyokua katika mchuano wao na Italia.

Aliiwaambia kuwa bidii yao yote waiweke katika mchuano huo moja, iwe ni kama fainali ya kombe la dunia kwao, kwani ikiwa watashindwa, itamaanisha kuondolewa kwao katika kombe la dunia.