Uholanzi kusonga mbele, Brazil

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Uholanzi ni timu ya kwanza kufuzu kwa mkondo wa pili wa kombe la dunia.

Uholanzi ilitoka mabao 2-1, nyuma na kuishinda Australia mabao 3-2 katika mchuano wa kusisimua wa kombe la dunia huko Rio de Janeiro, siku ya Jumatano.

Oranje kama inavyojulikana timu ya Uholanzi, iliiadhibu kwa urahisi Uhispania mabao 5-1 katika mchuano wao wa kwanza, lakini walilazimishwa kujikaza katika mchuano huu wa pili ilikupata ushindi.

Arjen Robben aliweka Uholanzi kifua mbele katika dakika ya 20.

Dakika moja baadaye, Australia walisawazisha kupitia mchezaji Tim Cahill.

Cahill baadaye alionyesha upande wake mbaya wakati alipomtendea dhambi Bruno Martins na kumfanya kuondolewa uwanjani katika machela.

Cahill aliadhabiwa na hili lamaanisha hatakuwa katika mechi inayokuja ya Australia dhidi ya Uhispania.

Mile Jedinak aliifungia Australia bao la pili kupitia penalti katika dakika ya 58 baada ya Daryl Janmaat kuugusa mpira ndani ya eneo lao la lango.

Robin van Persie pia alionyeshwa kadi ya njano kwa kumtendea visivyo Matthew Spiranovic, naye hatakuwa katika mchuano baina ya Uholanzi na Chile.

Hata hivyo katika aliifungia uholanzi bao la kusawazisha kunako dakika ya 68.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Uholanzi ni timu ya kwanza kufuzu kwa mkondo wa pili wa kombe la dunia.

Kuendelea kwa Uholanzi katika raundi ya pili ya kombe la dunia, bado kutaamulia katika mchuano wa mwisho kwani tofauti ya mabao yaweza kutatanisha.

Uholanzi inahitaji kushinda mechi hiyo ilikuepuka kuchuana na wenyeji brazil katika mkondo wa pili .

Mlinzi wa upande wa kulia wa Australia, Ryan McGowan aliupiga mpira uliowapita walinzi wa Uholanzi na kumfikia Cahill aliyeupiga ukagonga kizingiti cha juu ya lango la Uholanzi na kuingia.

Hili laweza kuawa moja kati ya mabao bora kabisa katika michuano hii.

Martins, aliyechezewa visivyo na Cahill, alibadilishwa na mchezaji Memphis Depay, nao Uholanzi wakabadilisha mchezo wao na kuanza kutumia mtindo wa 4-3-3.

Muda mfupi baadaye, Australia walijipata nyuma wakati mkwaju wa yadi 30, wake Depay ulimponyoka kipa wa Australia, Ryan, na kuingia.

Mkwaju wake Nigel de Jong pia ulizuiwa Uholanzi ikitafuta bao la nne.

Australia ilikua na nafasi pia ila haikuweza kupata bao la kusawazisha na matumaini yao ya kufika mkondo wa maondoano yakawa yanadidimia.