Ivory Coast 1-2 Colombia

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Gevinho alifungia Ivory Coast bao la kufutia machozi

Colombia ilipiga hatua kubwa ya kufuzu kwa raundi ya pili ya kombe la dunia baada ya kuilaza Ivory Coast mabao 2-1 katika mechi yao kali ya kundi C, iliyochezwa katika uga wa Estadio Nacional, Brasilia.

James Rodriguez aliiweka Colombia kifua mbele baada ya saa moja kupitia kichwa, naye mchezaji wa akiba Juan Quintero akongeza la pili.

Bao lake Gervinho liliwapa Ivory Coast matumaini.

Hata hivyo hawakuweza kusawazisha.

Timu zote mbili zilikua zimeshinda mechi zao za kwanza za ya kombe la dunia.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mfungaji bao la Colombia Rodriguez

Mkufunzi wa Colombia, Jose Pekerman alitumia kikosi kile kile alichokitumia katika mechi ya kwanza walipoishinda Ugiriki mabao 3-0.

Ivory Coast, tena walimwacha nje Didier Drogba akiuguza jeraha la paja, hata ingawa alicheza mchezo mzuri walipowashinda Japan 2-1 katika mechi yao ya kwanza huko Recife.

Ivory Coast sasa wanahitaji kushinda mechi yao ya mwisho dhidi ya Ugiriki ilikuwa na matumaini ya kumaliza katika nafasi ya pili ya kundi hilo na kusonga mbele katika hatua ya maondoano.

Colombia inaongoza kundi hilo ikiwa na jumla ya alama 6 huku Ivory Coast ikiwa ya pili na alama 3 kufuatia ushindi wao wa kwanza dhidi ya Japan.

Teofilo Gutierrez ndiye aliyetangulia kushambulia katika eneo la penalti la The Elephants wa Ivory Coast.

Mlinzi wa The Elephants, Didier Zokora alizuia shambulizi la Juan Cuadrado baadaye.

Haki miliki ya picha
Image caption Kibofu kilitupwa uwanjani na mashabiki wa Colombia

Serge Aurier, mlinzi wa Ivory Coast anayehusishwa na uhamiaji kwa timu ya Arsenal, alipiga shuti kutoka yadi 18 nao ukaokolewa kwa urahisi na kipa wa Colombia, David Ospina.

Katika kipindi cha pili, refa muingereza, Howard Webb, alikataa wito wa penalti kwa timu ya Ivory Coast baada ya Gervinho kuangushwa na Mario Yepes, nahodha wa Colombia.

Katika dakika ya 55, Zokora alionyeshwa kadi ya manjano baada ya kumkosea Cuadrado hivyo basi hataucheza mchuano wa mwisho wa makundi dhidi ya Ugiriki.

Colombia ilichukua uongozi katika dakika ya 64 baada ya mshambulizi wa Monaco, Rodriguez kufunga bao kwa kichwa baada ya kona.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mashabiki wa Colombia

Muda mfupi baada ya hapo, The elephants walifanya mabadiliko mengine.

Salomon Kalou aliingia katika nafasi ya Max Gradel.Hata hivyo, Colombia walifunga bao la pili katika dakika ya 70.

Gutierrez alimpa Juan Quintero pasi wawili hao walipoishambulia safu ya ulinzi ya Ivory Coast.

Quintero aliuchukua mpira nje ya eneo la penalti na kuupiga kwenye wavu wa The Elephants.

Dakika tatu baadaye, Gervinho alifunga bao lao la kufutia machozi, ambalo pia ni bao lake la pili katika michuano hii.

Ivory Coast sasa wanahitaji ushindi katika mechi yao ya mwisho dhidi ya Ugiriki ikiwa wana matumaini ya kuendelea mbele katika michuano hii ya kombe la dunia.

20:56 Colombia 2-1 Ivory Coast

20:56 Mpira umekwisha .

20:33 Gervinho anaifungia Ivory Coast

20:33 GOOOOOOOOAL

20:31 Juan Quintero anaihakikishia Colombia tikiti ya mkondo wa pili baada ya kosa la mlinzi wa Cote DIVoire

20:31Colombia 2-0 Ivory Coast

20:30 GOOOOOOOAL

20:25 Ivory Coast 0-1 Colombia 65''

20:25 James Rodriguez anafunga kwa kichwa

20:24 GOOOOOOAL

20:24 Kona kuelekea Ivory coast

20:22 Ivory Coast wanaboronga na kuruhusu mashambulizi ya Colombia

20:21 Colombia 0-0 Ivory Coast

20:20 Didier Drogba anaingia baada ya Bony kupumzishwa

20:17 Gradel na Bony wanatupa nafasi nzuri za kuifungia Ivory Coast mabao .

20:15 Zokora hatacheza mechi ya mwisho ya makundi dhid ya Ugiriki

20:14 Zokora anaoneshwa kadi ya njano na sasa ni Freekick kuelekea lango la Cote de Voire

20:12 Toure anapoteza fursa nzuri ya kuiweka Ivory Coast mbele sasa ni golkick

20:11 Freekick kuelekea lango la Colombia bada ya Toure kuangushwa.

20:08 Mkwaju wa Yaya Toure hautumiwi vyema na unanyakuliwa na Colombia

20:07 Freekick kuelekea lango la Colombia Gervinho ameangusha

20:07 Juan Guillermo Cuadrado anaendelea kutatiza safu ya kati ya Ivory Coast

20:05 kipindi cha pili kinaanza katika uwanja wa taifa ulioko Brasilia .

19:50 Colombia 0-0 Ivory Coast

19:48 Kipindi cha kwanza kimekamilika

19:42 Colombia 0-0 Ivory Coast 40''

19:39 Didier Zakora anautoa nje mpira na unakuwa wa kutupwa kuelekea lango la Ivory Coast.

19:38 Kona kuelekea upande wa Colombia unbadilika na kuwa shambulizi la Colombia .

19:36 Claudio Sanchez anapambana na Yaya Toure kuwania ubinga wa safu ya kati.

19:35 Freekick Kuelekea upande wa Ivory Coast lakini unaenda nje na inakuwa ni golkick!

Image caption Mashabiki wa Ivory Coast.

19:34 Yaya Toure anaanguka lakini Howard webb anasema endelea na mchezo

19:33 Orier anamjaribu kipa wa Colombia Ospina kutoka nje ya eneo baada ya kuona ukuta wao haupishi

19:31 Gutierez anakosa kuunganisha pasi safi sana akiwa amesalia na kipa pekee yake .

19:30 Colombia wanapoteza nafasi ya wazi ya kufunga bao lao la kwanza kutokana na FastBreak

19:29 Colombia 0-0 Ivory Coast 27''

19:28 Zuniga anatoa mpira nje na inakuwa Freekick kulekea Colombia

19:26 Kipa wa Colombia Ospina anawasuta walinzi wake wasiwaruhusu Ivory Coast kushambulia

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Ivory Coast inachuana na Colombia katika mechi yao ya pili ya kundi C

19:24 Gervinho anajibu shambulizi upande wa Ivory Coast

19:23 Boka ndiye anyeutoa m-pira nje

19:23 KONA kuelekea upande wa Ivory Coast

19:22 Colombia 0-0 Ivory Coast dakika ya 20

19:21 Mashambulizi kuelekea lango la Colombia

19:18 KONA kuelekea upande wa Ivory Coast .Zokora ndiye anayetoa mpira .

19:16 Tiote anamwangusha Cuadrado na inakuwa Freekick kuelekea Ivory Coast.

19:16 Mashambulizi sasa yanaelekea timu ya Ivory Coast

Image caption Kiungo wa kimataifa Toure anatarajiwa kushamiri katika safu ya kati.

19:15 Gervinho anakula chenga kali sana lakini mpira unatoka nje .

19:13 Yaya Toure ndiye anayeupiga lakini ukuta wa Colombia haupishi

19:12 Freekick kuelekea Colombia

19:12 Kona ya kwanza ya Ivory Coast lakini inazimwa na safuu ya ulinzi ya Colombia

19:00 Mechi imeanza Ivory coast 0-0 Colombia

19:00 Refarii katika mechi hii ya leo ni Howard Webb

18:59 Baada ya kubanduliwa kwa Cameroon matumaini ya bara la Afrika yanategemea matokeo ya leo ya Ivory Coast.

18:58Colombia iliilaza Ugiriki mabao 3-0 katika mechi yao ya kwanza

Image caption Drogba atarajiwa kungaa

18:57 Colombia sawa na Ivory Coast ilishinda mechi yake ya kwanza .

18:57 Ivory Coast ndiyo timu ya pekee kutoka Afrika iliyoshinda mechi yao ya kwanza dhidi ya Japan.

18:56 Timu zote zinaingia uwanjani.

18:56Ivory Coast inachuana na Colombia katika mechi yao ya pili ya kundi C