Suarez amng'ata Chiellini

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Suarez anashtumiwa kwa kumngata mlinzi wa Italia

Mshambulizi wa Uruguay Luis Suarez amekumbwa na kashfa mpya baada ya kuonekana kumngata Giorgio Chiellini wa Italia.

Suarez alionekana akiminya bega la Chiellini muda mchache kabla ya Diego Godin kufunga bao la ushindi la Uruguay dhidi ya Italia.

Chiellini aliangushwa chini na uchungu wa meno ya Suarez na alionekana akimkimbilia refarii akimvulia shati ilikuonesha alama ya meno begani lakini refarii akapuzilia mbali .

Chiellini ameiambia runinga moja ya Italia kuwa Suarez alijiangusha chini likuficha uovu huo wa kutisha na kusingizia kuwa alikuwa amepigwa kumbo.

Image caption Suarez anatumumiwa kwa kumngata Chielleini

Suarez alionekana akigaaga uwanjani baada ya tukio hilo.

Japo refarii Marco Rodriguez hakuona tukio hilo la kutamausha Chiellini amesikika akisema kuwa ni jambo la kuhuzunisha kuwa refarii huyo alipuzilia mbali maombi yake ya kutaka hatua ichukuliwe dhidi ya mshambulizi huyo ambaye aliadhibiwa kwa tukio lengine kama hilo akiichezea Liverpool misimu miwili iliyopita nchini Uingereza.

Suarez alilazimika kukaa nje kwa mechi 10 baada ya kumngata kiungo wa Chelsea Branislav Ivanovic aprili 2013.

Image caption Suarez na refarii wa mechi hiyo Marco Rodriguez

Awali Suarez aliadhibiwa na shirikisho la soka la Uholanzi lilimuadhibu Suarez kwa marufuku ya mechi saba baada ya kumngata mchezaji wa PSV Eindhoven Otman Bakka wakati huo akiwa nahodha wa Ajax Amsterdam.

Mwaka wa 2010 Suarez aliunawa mkwaju ambao ulikuwa unaingia wavuni na kuinyima Ghana nafasi ya kuingia kwenye nusu fainali ya kombe la dunia .