Iran 1-3 Bosnia H

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Iran na Bosnia-Hercegovina zimeaga mashindano huko Brazil

Matumaini ya Iran ya kufuzu katika hatua ya pili ya timu 16 bora katika Kombe la Dunia yalizimwa na Bosnia-Hercegovina ambao tayari waalikuwa wamekwisha ondolewa.

Iran ilikuwa inahitaji ushindi wa aina yeyote na kuomba kuwa Nigeria iambulie kichapo hata hivyo Edin Dzeko alizima matumaini yeyote ya kusonga mbele alipoifungia Bosnia bao la kwanza kwa mkwaju aliopiga kutoka nje ya yadi 25.

Mchezaji wa Roma Miralem Pjanic alifunga la pili baada ya mapumziko.

Reza Ghoochannejad aliifungia Iran bao la kufutia machozi kabla ya Avdija Vrsajevic kuongeza bao la tatu na la ushindi .

Huu ndio uliokuwa ushindi wao wa kwanza katika Kombe la Dunia.

Upande wao Safet Susic walikuwa tayari washabanduliwa kutoka kwa kipute hicho kabla ya mechi ya Jumatano baada ya kushindwa na Argentina na Nigeria katika mechi yao ya ufunguzi.

Bao lake Dzeko dhidi ya Iran lilimfariji hasa baada ya bao lake dhidi ya Nigeria kukataliwa kimakosa wakati walipokuwa bado haawajafungana.

Iran ilihitaji ushindi na kuomba kwamba Nigeria ingeshindwa ili ifuzu, na walianza kushambulia mara tu mechi hiyo ilipoanza .

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Iran na Bosnia-Hercegovina zimeaga mashindano huko Brazil

Masoud Shojaei akatikisa mlingoti chini ya dakika moja tangu Bosnia ilipofunga.

Lingekuwa bao lao la kwanza katika Kombe la dunia tangu walipotoka sare ya bao 1-1 na Angola mwaka wa 2006.

Kocha wa Bosnia Safet Susic: alisema alifarijika na ushindi dhidi ya Iran huku Kocha wa Iran Carlos Queiroz: akitania kwa kusema "Timu bora Zaidi katika kundi haikufuzu, Bosnia ilionyesha kuwa ina wachezaji wazuri, timu nzuri yenye tajriba chungu nzima.

“Leo walipandisha kiwango chao na wakati huo hawakutupa nafasi.

“Wachezaji wangu walicheza vizuri sana, na ninajivunia sana, sana, najivunia sana.”