Costa Rica kuchuana dhidi ya Ugiriki

Image caption Costa Rica kuchuana na Ugiriki

Mechi baina ya Costa Rica na Ugiriki ni moja kati ya mechi ambazo hazikutarajiwa na asilimia kubwa ya wapenzi wa kandanda na haswa kombe la dunia .

Asili mia kubwa ya wapenzi wa soka walipigia upatu Uhispania Uholanzi Argentina na Ubeljiji kutwaa kombe la mwaka huu Brazil2014.

Lakini baada ya mbivu na mbichi kubainika katika mechi za mchujo wa raundi ya kwanza Ugiriki imo katika raundi ya pili.

Ugiriki ilifuzu baada ya kuizidi maarifa Ivory Coast na Japan siku ya mwisho ya mechi hizo za makundi.

Ugiriki itakuwa na nahodha wao Kostas Katsouranis ambaye alikosa kucheza mechi yao dhidi ya Ivory Coast kwani alikuwa akitumika marufu baada ya kupokea kadi mbili za manjano.

Kocha wa Ugiriki Fernando Santos amemlimbikizia sifa Costa Rica kwa kushinda mechi zao zote katika kundi la Kifo .

Haki miliki ya picha AP
Image caption Costa Rica kuchuana na Ugiriki

Santos anasema kwa timu kuibuka kidedea katika kundi linalojumuisha waliokuwa mabingwa wa dunia Uingereza na Italia basi sio timu ya kuitweza .

Santos hata hivyo alikanusha madai kuwa Ugriki inapenda kujaza safu ya ulinzi badala ya kucheza mfumo wa nipe nikupe .

Costa Rica ilikamilisha mechi zake za makundi bila ya kushindwa .

''Sharti Costa rica ipewe heshma yake kwa namna walivyozisambaratisha upinzani katika kundi hilo la Kifo.''

Costa Rica waliibua mjadala kote duniani baada ya kuibana Italia na kisha kuinyeshea Uruguay 3-1 .

Timu hiyo inatarajiwa kuichezesha kikosi kizima kilichoishinda Italia katika mechi ya pili ya makundi.

kikosi hicho kitajumuisha mlinzi Michael Umana na kiungo cha kati Christian Bolanos wakirejea uwanjani baada ya kukaa nje katika mechi yao ya mwisho.