Costa Rica kuchuana na Uholanzi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Costa Rica kuchuana na Uholanzi baada ya kuilaza Ugiriki 5-3 kupitia penalti

Costa Rica imefuzu kwa robo fainali ya kombe la dunia baada ya kuilaza Ugiriki mabao 5-3 kupitia mikwaju ya penalti katika mechi ngumu iliyochezewa Recife.

Costa Rica ilicheza zaidi ya saa nzima ikiwa na wachezaji kumi uwanjani baada ya Oscar Duarte kuoneshwa kadi ya pili ya njano alipomwangusha Jose Holebas kunako dakika ya 62.

Sokratis Papastathopoulos aliifungia bao la kusawazisha dakika ya mwisho ya muda wa kawaida na hivyo kuihakikishia ugiriki dakika 30 zaidi kuamua iwapo watachuana na Uholanzi au la katika awamu ijayo ya nane bora ama ukipenda robo fainali ya kombe la dunia mwaka huu .

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Costa Rica kuchuana na Uholanzi baada ya kuilaza Ugiriki 5-3 kupitia penalti

Bryan Ruiz ndiye aliyekuwa ameiweka the Tico's mbele kunako dakika ya 52 .

Kufuatia Ushindi huo wa kihistoria The Ticos ,sasa watachuana na Uholanzi siku ya jumamosi baada ya Uholanzi kufaidi penalti katika muda wa majeruhi ya kipindi cha pili na kuinyuka Mexico mabao 2-1.

Costa Rica itamshukuru kipa machchari Keylor Navas kwa tikiti hiyo ya nane bora baada yake kuokoa mikwaju mingi tu ya mashambulizi ya Ugiriki lakini kwa kina haswa kwa kuzuia kombora la Theofanis Gekas

lililotofautisha mbivu na mbichi katika mechi hiyo.