Algeria 1-2 Ujerumani

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wafungaji mabao ya Ujerumani Mesut Ozil na Andre Schurrle

Mechi imekamilika . Ujerumani 2-1 Algeria .

Ujerumani sasa itachuana na Ufaransa katika robo fainali ya kombe la dunia katika uwanja wa Marakana.

Afrika sasa haina mwakilishi katika robo fainali ya kombe la dunia la mwaka wa 2014 baada ya wawakilishi wenza wa bara la Afrika katika mkondo wa pili Nigeria kushindwa mabao mawili kwa nunge na Ufaransa katika mechi iliyotangulia .

Kufutatia ushindi huu wa Ujerumani ni dhahiri sasa kuwa timu zote zilizoongoza baada ya mechi za makundi ndizo zilizofuzu kwa robo fainali ya kombe la dunia .

Ufaransa itakabiliana na Ujerumani siku ya ijumaa katika uwanja wa Maracana saa moja usiku saa za Afrika Mashariki.

Mechi itatangulia ile kati ya weneyeji Brazil na Colombia.

Jumamosi ijayo Uholanzi itakuwa na kibarua kiguimu dhidi ya Costa Rica

30:00+01 GOOOOOAL Ujerumani 2-1 Algeria Djabau

30:00 Ujerumani imefuzu kwa robo fainali

30:00 Ujerumani 2-0 Algeria Mesut Ozil

Image caption Ujerumani 1-0 Algeria 20''

17:50 Kipa wa Ujerumani Nuer anaudaka bila wasiwasi.

16:30 FREEKICK kuelekea upande wa Ujerumani na mpira unapigwa na Ibrahimi

15:30 Kipindi cha pili kimeanza kwa kasi kama kile cha kwanza lakini wanaofanya mashambulizi sasa ni Algeria .

15:00 Ikiwa mechi hii itaisha ikiwa hivi,basi inaonesha kuwa timu zote zilizoshinda makundi yao ndizo zilizoshinda mechi za mkondo wa pili.

15:00+01 Kipindi cha kwanza cha muda wa ziada kimekamilika Ujerumani 1-0 Algeria

15:00+01 Algeria wanaonekana kukubali hatima ya mechi hii

15:00 Kipindi cha kwanza kimekamilika .

13:40 Moustafa anajaribu kupenya safu ya ulinzi ya ujerumani lakini wapi

12:50 Mpira unatolewa nje na Aissa Mandi

11:00 KONA kuelekea lango la Ujerumani

02:50 André Schürrle''02 ET anaifungia Ujerumani bao lao la kwanza

02:00 GOOOOOOOAL Ujerumani 1-0 Algeria

ETRATIME

90:00+4 Mechi imekamilika Algeria 0-0 Ujerumani .Mechi hii sasa itaamuliwa katika muda wa zaida

89:00 Ujerumani inaendelea na mashambulizi lakini Algeria inahimili mikiki yao.

86:00Freekick kuelekea lango la Algeria nje tu ya eneo

Image caption Muller anakosa nafasi ya wazi

85:14

85:00 Muller anakosa fursa ya wazi

Image caption Nuer analazimika kuisadia safu yake ya ulinzi

74:30 Slimani anamjaribu Nuer kuitoka mbali lakini wapi ,Boateng anazuia duh!

71:48 Freekick baada ya Muller kuangushwa nje ya eneo

70:00 Kipa wa Ujerumani anafanya kazi ya ziada kuzuia shambulizi la Algeria.

Image caption Kipa wa Algeria anafanya kazi ya ziada

65:00

61:40 Kona kuelekea lango la Algeria ,Inapigwa na Kroos na shambulizi linazimwa .

60:00 Ujerumani 0-0 Algeria ''60

58:02 Nipe nikupe katikati ya uwanja lakini ujerumani wakionesha ukakamavu wao

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ujerumani 0-0 Algeria 62''

54:50 Shambulizi linazimwa baada ya kipa wa Algeria Rais kuutema

54:20 Kona kuelekea lango la Algeria

52:13 Andre Schurrle anapoteza nafasi nzuri mbele ya lango la Algeria .

48:41 Ujerumani wanaonekana wamechochewa kushambulia lango la Algeria

Image caption Algeria 0-0 Ujerumani 55

47:30 Kona kuelekea lango la Algeria .

46:30 Ujerumani 0-0 Algeria

46:00Kipindi cha pili kimeanza tena.

45:00+1 kipindi cha kwanza kimekamilika timu zote zikiwa hazijapata bao lolote

Image caption Kroos akishambulia Rais Mbolhi

45:10 Freekick Kuelekea lango la Ujerumani

44:50 Toni Kroos anatuma kombora lakini nje .

44:50 Algeria 0-0 Ujerumani

Image caption jaribio lingine katika lango la Algeria

41:15

37:00 Kipa wa Algeria anautema mpira mbele ya lango ,,,Nusura Muller atume kombora lakini unatoka nje na ni Goal Kick kuelekea lango la Ujerumani

36:00 Algeria wanawadhibiti Wajerumani hatua kwa hatua katika mechi hii

33:00 Leohart Frasha Lavendar matumaini ya mende kubeba kabati..,hahaha

33:00 Frank Mshana wa Tz anasema Ubinafsi ndio unatuangusha

31:10 Free kick kuelekea lango la Ujerumani nje ya eneo

30:00 Ujerumani 0-0 Algeria

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Boateng na mpira !

28:30

24:45 Muller na Boateng wanashirikiana kumpokonya Soudani mpira .

23:50 Inazimwa kwa kicha na sasa imemfikia Ozil na Ujerumani wanapanga shambulizi lengine

22:30 Ujerumani inapata KONA

Image caption Slimani anapoteza nafasi nyengine alikuwa ameotea

20:45 Mechi inavyoendelea inaonesha timu zote zimetoshana nguvu

17:50 Zidane na slimani wanapoteza nafasi nyengine ya wazi mbele ya lango la Ujerumani

16:20 OFFSIDE Bao la Algeria linakataliwa kwa kuwa Slimani alikuwa keshaotea .

15:30 Ujerumani 0-0 Algeria

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mashabiki wa Algeria

12:40

10:30 Algeria Inashambulia lango laUjerumani ikibainika kuwa Slimani anamshinda kwa kasi Per Mertesacker .

08:40 Algeria wanageuza ulizni kuwa shambulizi linalomlazimu kipa wa Ujerumani kuondoka langoni ili kuzuia mashambulizi Islam Slimani

07:43 Shambulizi kuelekea upande wa Algeria .

02;50 Offside ya kwanza kuelekea upande wa Algeria .

01 Mpira unaanza uwanjani Porto Alegre

Image caption Algeria inabeba matumaini ya Afrika inapochuana na Ujerumani katik mechi ya mwisho ya mkondo wa 16 bora.

Wimbo wa taifa unachezwa

Algeria inabeba matumaini ya Afrika inapochuana na Ujerumani katik mechi ya mwisho ya mkondo wa 16 bora.

Mshindi atachuana na Ufaransa ambayo iliizima Nigeria 2-0

Mara ya mwisho Algeria iliilaza ujerumani Magharibi mabao 2-1

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Algeria inakabiliana na Ujerumani.

Hii ni Mara ya kwanza kwa Algeria kuchuana na Ujerumani tangu mwaka wa 1982