Kocha wa Nigeria Keshi amejiuzulu

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kocha wa Nigeria Keshi amejiuzulu

Kocha wa Nigeria coach Stephen Keshi amejiuzulu wadhfa wake katika timu hiyo .

Keshi amejiuzulu punde baada ya timu ya Super Eagles kuondolewa kutoka kwenye kipute cha kombe la dunia ilipolazwa 2-0 na Ufaransa .

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 alichukuwa wadhfa huo mwaka wa 2011 na akaiongoza timu hiyo kufutwaa ubingwa wa afrika mwaka uliopita .

Nahodha wa timu hiyo Joseph Yobo aliyejifunga bao la pili la Ufaransa naye pia ametangaza kustaafu .

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Keshi kujiuzulu wadhfa wakae,mwaka wa 2013 Keshi alikuwaradhi kujiuzulu lakini akashawishiwa kusalia kama kocha na waziri wa michezo wa Nigeria.

Chini ya uongozi wake Super Eagles imefuzu kwa mara ya kwanza katika mkondo wa pili wa kombe la dunia tangu mwaka wa 1998 licha ya kukumbwa na migomo ya mara kwa mara ya wachezaji wake wakidai malimbikizi ya marupurupu yao.

Kuondoka kwake kumefikisha idadi ya wakufunzi waliojiuzulu kufuatia matokeo duni katika kombe la dunia kutimia makocha 6.

Makocha wengine waliondoka ni pamoja na Luis Suarez, wa Honduras, Carlos Queiroz wa Iran's , Alberto Zaccheroni wa Japan , Cesare Prandelli wa italia na Sabri Lamouchi wa Ivory Coast.

Keshi, aliwahi kuhudumu kama kocha wa Mali na Togo.