Argentina 1-0 Uswissi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mfungaji bao la ushindi la Argentina Di Maria

Argentina ilijikatia tikiti ya robo fainali baada ya ya kusubiri hadi muda wa ziada kuibana Uswisi kwa bao moja kwa nunge.

Timu hizo zilikuwa zimetoka sare tasa katika dakika 90 za mechi hiyo kabla ya Angel Di Maria kufunga bao la pekee na la ushindi zikiwa zimesalia dakika mbili za muda huo wa ziada kukamilika .

Bao hilo lilikuwa la 151 katika kipute hichi ikilinganishwa na mabao 145 yaliyofungwa katika kinyang'ari cha miaka minne iliyopita huko Afrika Kusini.

Ijapokuwa nyota wa Barcelona Lionel Messi alikuwa amepigiwa upatu kushamiri katika mechi hii mshambulizi huyo ambaye amefunga bao katika kila mechi alikuwa amekabwa na walinzi wa Uswisi wakiongozwa na Behrami.

Kocha wa Uswisi Ottmar Hitzfeld, alikuwa amepanga kikosi chake kumnyima nafasi yeyote Messi lakini nyota huyo ali geuka na kuwa anagawa mipira alipommegea pasi safi Di Maria .

Image caption Mfungaji bao la ushindi la Argentina Di Maria

Awali nafasi nyingi tu za mashambulizi ya Uswisi yaliambulia patupu Shakiri alipokosa mpenyo katika safu ya ulinzi ya Argentina.

Granit Xhaka alipoteza nafasi safi ambayo waswisi watajilaumu wenyewe haswa baada ya Josip Drmic kujipata katika hali ya moja kwa moja na kipa wa Argentina Sergio Romero .

juhudi zake hata hivyo ziliambulia mikononi mwa Romero.

Kufuatia ushindi huo Argentina sasa watachuana dhidi ya Ubeljiji katika mechi ya robo fainali ya kombe hilo la dunia jumamosi tarehe 5 Julai .

Ubeliji imejikatia tiketi ya robo fainali hiyo baada ya kuititima Marekani mabao mawili kwa moja katika muda wa ziada wa mechi hiyo ya mwisho ya kundi la 16 bora.