Ni vita vikali Argentina vs Ubelgiji

Haki miliki ya picha Reuters

Katika historia za kukutana Argentina imeshinda mara tatu katika mara nne zilipokutana wakati Ubelgiji ikishinda mara moja mwaka 1982 kwa kuifunga Argentina kwa goli 1 - 0 katika hatua ya makundi.

Argentina ilitolewa mara tatu ya mwisho katika hatua ya robo fainali. Ilipoteza dhidi ya Ujerumani mwaka 2010 na dhidi ya Uhalanzi mwaka 1998 na baadae ikatolewa na Ujerumani mwaka 2006 kwa mikwaju ya penalti.

Ukiachilia mbali kuondolewa kwa mikwaju ya penalti, Argentina haijawahi kushinda kwenye hatua ya robo fainali tangu ilipoifunga England mwaka 1986 magoli 2 -1.

Tegemeo la Argentina kwa sasa Lionel Messi ambaye amefunga au kusaidia kufungwa kwa magoli matano kati magoli saba Argentina iliyofunga katika kombe la dunia la mwaka huu 2014.

Magoli matatu ambayo Messi aliyafunga manne aliyafunga nje ya kisanduku cha kumi na nane.

Kwa upande wa Ubelgiji hii ni mara ya pili kwao kufikia hatua ya robo fainali. Mara ya mwisho iliifunga Uhispania mwaka 1986 kuingia hatua ya nne bora.

Mwamuzi: Nicola Rizzoli