Shabiki wa Brazil auawa Kenya

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mashabiki wawili wauawa Kenya kufuatia ushindi wa Brazil dhidi ya Colombia

Furaha ya mashabiki wawili wa kombe la dunia iligeuka na kuwa matanga jumamosi usiku baada ya watu wawili kupoteza maisha kufuatia ubishi kuhusiana na matokeo ya kombe la dunia linaloendelea huko Brazil.

Shabiki wa kwanza aliuawa baada ya utani wa shabiki ilizusha ubishiuliyosababishwa akadungwa kisu tumboni nje ya baa moja katika mtaa wa Awendo iliyoko katika jimbo la Migori magharibi mwa Kenya.

Afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo,Kipsang Chengach alisema kuwa wawili hao walikuwa washabikia timu hasimu katika mechi hiyo ya robo fainali kati ya Brazil na Colombia na baada ya Brazil kushinda mmoja akamdunga mwenzake kisu na kisa akatoroka.

Zaidi ya Saa nane baadaye yule aliyetoroka eneo la tukio naye alisakwa na umati wa watu waliokuwa wamejawa na hamaki na wakampiga hadi kufa kabla ya polisi kufika huko alikokuwa ametorokea.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mashabiki wawili wauawa Kenya kufuatia ushindi wa Brazil dhidi ya Colombia

Shabiki mmoja aliyeshuhudia matukio hayo aliwaambia polisi kuwa alishuku alikuwa ameweka dau na akashindwa kulipa baada ya mechi hiyo ambayo Brazil iliibuka washindi mabao 2-1.

Miili yote miwli imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya.