Djokovic amzima Federer Wimbledon

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Djokovic ndiye bingwa wa Wimbledon

Mchezaji tenis wa Serbia Novak Djokovic ndiye bingwa wa mwaka huu wa kombe la Wimbledon.

Djokovic alimlaza Mswisi Rodger Federer seti tatu kwa mbili za alama 6-7 (7/9), 6-4, 7-6 (7/4), 5-7, 6-4 katika fainali hizo za wanaume..

Bingwa huyo wa mwaka wa 2011 alitamatisha msururu wa kushindwa kwa mataji makuu ya Grand Slam alipoandikisha taji lake kuu la 7 .

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Djokovic ndiye bingwa wa Wimbledon

Mchezji huyo mwenye umri wa miaka 27 alishangilia ushindi huo wa kihistoria kwa kupigasijida katikati ya uwanja wa kati huko wimbledon na kutafuna nyasi asijue aliwahi vipi kumkomesha federer ambaye alikuwa anatafuta taji lake la nane na la kuvuweka rekodi mpya.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Djokovic alimshinda Federer katika fainali za Wimbledon

Iwapo angeshinda Federer angekuwa ndiye mchezaji mkongwe zaidi kuwahi kutaa ubingwa huo akiwa na umri wa miaka 32 .

Rekodi ya sasa inashikiliwa na Pete Sampras ambaye ameshinda mataji saba sawa na Federer.