Webb huenda akaamua fainali Brazil

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Refarii Howard Webb

Referii muingereza anayefahamika kwa ukakamavu wake Howard Webb ni miongoni mwa waamuzi 15 walioteuliwa kusalia Brazil kushiriki mechi zilizosalia za kombe la dunia.

Webb mwenye umri wa miaka 42 ni miongoni mwa wale watakaotathminiwa kwa uwezo wao wa kuamua mechi zenye umuhimu mkubwa ikiwemo fainali ya kombe la dunia huko Brazil.

Webb pamoja na wasaidizi wake Mike Mullarkey na Darren Cann wamekwisha amua mechi mbili za kombe la dunia huko Brazil.

Image caption Webb ni kati ya waamuzi 15 waliosalia Brazil

Mpiga kipenga huyo alikuwa muamuzi katika mechi kati ya Colombia na Ivory Coast na pia mechi baina ya wenyeji Brazil na Chile.

Webb alijiimarisha wasifu wake mwaka wa 2010 alipoamua mechi ya fainali ya kombe la dunia baina ya uhispania na Uholanzi nchini Afrika Kusini .

Image caption Webb ndiye aliyeamua fainali ya kombe la dunia la mwaka wa 2010

Webb hata hivyo alilaumiwa kwa kukosa kumwadhibu mchezaji Nigel de Jongfor .

Na baada ya kutizama kanda za video Webb alikiiri kuwa alistahili kumwonesha mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United kadi nyekundu .

Refarii mmoja pekee kutoka Brazili, Sandro Ricci ndiye aliyesalia kuamua mechi zilizosalia za nusu fainali fainali na mechi ya kuamua mshindi wa tatu.

Mbali na Brazili Argentina, Ujerumani na Uholanzi ndiyo mataifa yaliyosalia katika kipute hicho.

Image caption Refarii Marco Rodriguez ndiye aliyakosa tukio la Suarez kumng'ata Chiellini

Refarii kutoka Mexico Marco Rodriguez ndiye atakayeamua mechi ya kwanza ya nusu fainali kati ya Ujerumani na wenyeji Brazil.

Mechi hiyo itachezwa Jumanne .

Rodriguez ndiye refarii ambaye alikosa kumuona mshambulizi wa Uruguay Luiz Suarez akimng'ata mlinzi wa Italia Giorgio Chiellini.