Baada ya Neymar sasa ni Van Persie

Image caption Hofu kuwa Van Persie huenda asishiriki mechi dhidi ya Argentina

Kocha wa Uholanzi Lous van Gaal amezua taharuki baada ya kusema kuwa mashambulizi wake matata van Persie anaugua utumbo na kuwa anahofu iwapo atacheza dhidi ya Argentika katika mechi ya pili ya nudu fainali au la.

Kocha Van Gaal amesema kuwa nafasi yake huenda ikachukuliwa na Nigel de Jong iwapo daktari wa timu hiyo atadhibitisha kuwa van Persie huenda akashindwa kuhimili uchungu na hivyo kukosa mechi hiyo muhimu.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Je van Persie atacheza dhidi ya Argentina ?

Iwapo de Jong atacheza basi itakuwa mara yake ya kwanza tangu aondoke uwanjani katika mechi ambayo Uholanzi iliilaza Mexico mabao 2-1 katika raundi ya kwanza.

Kocha huyo anakila sababu ya kuwa na wasiwasi baada ya Nahodha wake kutoshiriki mazoezi siku ya kuamkia mechi hiyo muhimu , hata hivyo anaafueni baada ya kurejea kwa Ron Vlaar na Leroy Fer mazoezini.

wawili hao walikuwa wamejeruhiwa katika mechi za makundi.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Argentina inamtegemea Messi kuifungia mabao

Kwa upande wao Argentina wnaendelea na mazoezi yao kikamilifu ijapokuwa inatarajiwa kuwa Mshambulizi wa Bracelona Lionell Messi atakabidhiwa majukumu mahsusi ya kuifikisha Argentina katika fainali yao ya kwanza tangu mwaka wa 1990.

Argentina pia wanatatizika kwa kumkosa mchezaji wa kutegemewa Angel Di Maria ambaye amejeruhi paja lake lakini watakuwa na wasaidizi wake Sergio Aguero na Marcos Rojo ambao watakuwa kwa ajili ya mechi hiyo ya kihistoria kwao.

Uholanzi tofauti na Argentina imefuzu kwa fainali ya kombe la dunia mara mbili zilizopita ikimaliza ya pili mara mbili mfululizo .