Ghana yakana wakimbizi Brazil

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Black Stars ya Ghana .

Serikali ya Ghana imehuzunishwa na kashfa ya zaidi ya mashabiki 200 wa taifa hilo waliomba hifadhi nchini Brazil wakidai kuwa walikuwa ni Wakristu waliokwepa mapigano ya kidini dhidi ya Wasilamu.

Katika Taarifa kwa Wanahabari, Serikali ya Ghana imesema kuwa hakuna vita vyovyote vya kidini nchini humo .

Kikundi hicho kilichopelekwa Brazil na serikali ilikuwashabikia Black Stars ya Ghana ilipokuwa ikishiriki mchuano wa kombe la dunia kilikataa kurejea makwao baada ya Ghana kubanduliwa nje ya kipute hicho.

Kulingana na Utafiti wa Shrika moja la Marekani Ghana ndilo taifa linaloonekana dhabiti na lenye kushuhudia amani katika Magharibi mwa bara Afrika.

Naibu waziri wa habari nchini humo bwana Felix Kwakye Ofosu amekanusha madai ya mashabiki hao akisema wizara ya mashauri ya kigeni ya Ghana imeanza kuchunguza madai hayo na kuwa hatua mahsusi zitachukuliwa karibuni.

Haki miliki ya picha s
Image caption Mashabiki wa Ghana huko Brazil

Polisi nchini Brazil walitoa tahadhari mapema wiki hii kuwa wanawatarajia takriban raiya 1000 kutoka Ghana kuomba hifadhi ya ukimbizi nchini humo punde baada ya kukamilika kwaa kipute cha kombe la dunia .

Maafisa wa uhamiaji wa Brazil wanasema tayari wamepokea maombi katika mji wa kifahari wa Caxias do Sul ulioko kusini mwa nchi hiyo.

Eneo hilo la Serra Gaucha - linajulikana kwa ufanisi wake na kuwa Mamia ya Waghana wanatarajiwa kuomba ruhusa ya kufanya kazi kulingana na afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo Noerci da Silva Melo.

Lakini waziri wa michezo wa Ghana Mahama Ayariga ameiambia BBC kuwa licha ya kuwa walioamba hifadhi ni sehemu ya mashabiki 650 waliopelekwa Brazil kuishangilia Black Stars taifa hilo linakisia kuwa njama ya kuiaibisha tu kwani Ghana haijashuhudia mapigano ya aina yeyote ya Kidini

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Baadhi ya Mashabiki wa Ghana wameomba hifadhi ya Ukimbizi Brazil

Mji wa Caxias do Sul uko zaidi ya Kilomita 1,600 km kutoka mji uliokuwa mwenyeji wa mechi zilizojumuisha Ghana yaani Natal Fortaleza na Brasilia.

Kanisa Katoliki tayari limewapatia makao wale ambao maombi yao yalikubalika .