Je Waingereza waogopa vilabu vya nje?

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mlinzi wa zamani wa Arsenal na Chelsea, Cole aelekea klabu ya Roma Uitaliano

'Waingereza hawapanii kuchezea vilabu vya nje'- asema Ashley Cole

Mlinzi huyo wa zamani wa Arsenal na Chelsea, mwenye umri wa miaka 33, amesema kuwa wanasoka wa Uingereza wanaogopa kujisajili katika vilabu vya nje ya Uingerea - kwanini ?

Adai wanahisi wametulia tuliii nyumbani hivyo hawataki au hawawezi bughdha za vilabu vya ugenini.

Yeye mwenyewe Ashley, anahamia Roma Uitaliano wakati mkaba wake na Chelsea unapokamilika.