Je TZ itamaliza ukame mwaka huu?

Image caption Fabian Joseph alishinda shaba mwaka 2006

Katibu Mkuu wa kamati ya Olympiki ya Tanzania Filbert Bayi ametangaza kikosi cha wanamichezo 37 na maafisa 10 watakaoiwakilisha Tanzania kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow, Scotland, kuanzia Julai tarehe 23.

Mkuu wa kikosi hicho ni mkurugenzi wa michezo nchini Tanzania Leonard Thadeo.

Tangu michezo ya Jumuiya ya Madola mwaka wa 2006 Tanzania iliposhinda medali mbili - dhahabu kupitia Samson Ramadhan na shaba ya Fabian Joseph Naali - Tanzania haijashinda medali tena kwenye michezo hii.

Je, mwaka huu unaona Tanzania itazoa dhahabu nyingi zaidi mjini Glasgow? toa maoni yako katika ukurasa wetu wa Facebook: https://www.facebook.com/pages/BBC-Swahili/160894643929209