England yashuka daraja hadi 20- Fifa

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Wachezaji mahiri wa England kama Rooney walishindwa kung'ara katika kombe la dunia

Timu ya Uingereza imeshuka ngazi ya orodha ya Fifa hadi nambari 20,nafasi ya chini zaidi tangu miaka ya 90.

Kushuka huko kwa karibu nafasi 10 chini.

Hii ni baada ya matokeo mabovu katika kombe la dunia Brazil 2014.

Sasa wako nyuma ya timu kama Bosnia-, Costa Rica hata Marekani.

Uhispania imeshuka kutoka namba moja hadi nane.

Bila shaka vinara ni ujerumani na nafasi nyingi kwenye kumi bora zimenyakuliwa na timu za mataifa ya Marekani kusini. Argentina, Brazil, Colombia, Uruguay , Costa rica na kadhalika.