Rodriguez atua Bernabeu kwa miaka 6

Haki miliki ya picha Real Madrid
Image caption Real Madrid imemnunua James Rodriguez

Mshambulizi wa Colombia na Monaco James Rodriguez amezunduliwa kama mchezaji wa Real Madrid baada ya kutia sahihi kandarasi ya miaka 6 na mabingwa hao wa bara Ulaya.

Mchezaji huyo wa aliyetwaa taji la mfungaji mabao mengi katika kombe la dunia huko Brazil ameandikisha kandarasi ya miaka 6 na klabu hiyo.

Duru zinaiarifu BBCMichezo kuwa huenda James akapokea kitita cha dola milioni mia moja.

Kutua kwake huko Bernabeu kumemuweka Rodriguez katika mizani sawa na Gareth Bale, Cristiano Ronaldo na Luis Suarez.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Real Madrid imemnunua James Rodriguez

Iwapo Rodriguez atalipwa takriban pauni millioni 80 basi huenda atakuwa mchezaji wa nne ghali zaidi nyuma ya Bale, Ronaldo na Suarez.

Rodriguez aligonga vichwa vya habari baada ya kutinga mabao 6 licha ya timu yake ya Colombia kubanduliwa nje ya kombe la dunia katika hatua ya robo fainali.

Rodriguez alifunga mabao dhidi ya Ugiriki , Ivory Coast na Japan lakini atakumbukwa zaidi kwa bao lililopigiwa upatu kuwa bora zaidi katika mashindano hayo dhidi ya Uruguay.

Kabla ya kujiunga na Monaco Rodriguez alikuwa amedhihirisha udeddea wake huko Ureno alikotwaa mataji matatu ya ligi akiwa na klabu ya Porto.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Real Madrid imemnunua James Rodriguez

Naibu mwenyekiti wa wa klabu ya Monaco Vadim Vasilyev alisewaambia wanahabari kuwa klabu hiyo haikuwa na niya ya kumuuza mshambulizi huyo lakini hawakutaka kupitwa na kitita kikubwa kilichotolewa kwao na kumweka katika mizani sawa na washambulizi ghali zaidi katika hstoria ya kandanda.

Madrid ilitoa kitita cha pauni milioni 80 kumnunua Ronaldo alipotokea Manchester United mwaka wa 2009.

Na ulimwengu na kandanda ulipodhania kuwa historia hiyo haingevunjwa Madrid ilitoa pauni milioni 85.3m mwaka uliopita na kumnunua Bale kutoka kwa Tottenham ya Uingereza.