FIFA yaafiki marufuku ya mGhana

Image caption Fifa imempiga marufuku Mark Edusei kwa kupanga mechi

Mchezaji wa zamani wa timu ya Black Stars ya Ghana Mark Edusei amepigwa marufuku kushiriki aina yeyote ya mchezo wa kandanda kote duniani na shirikisho la soka duniani FIFA.

Edusei alikuwa amepigwa marufuku ya kutoshiriki mashindano yeyote ya kandanda na shirikisho la soka la Italia (IFF) pia mahakama ya rufaa ikaafiki uamuzi huo mwezi mei.

Mchezaji huyo wa zamani wa Black Stars alipatikana na hatia ya kupanga matokeo ya mechi ya serie B tarehe 23 mwezi Mei 2009 ambapo timu yake ya Bari iliambulia kichapo cha mabao 3-2 dhidi ya Salernitana.

Edusei, aliwahi kuichezea Ghana katika kombe la kuwania ubingwa wa Afrika la mwaka wa 2000 .

Mechi yake ya mwisho ilikuwa mwaka wa 2011 katika klabu moja ya Uswissi mwaka wa 2011.

Edusei aliwahi kuichezea klabu ya Sampdoria na Torino .