Lukaku asajiliwa Everton

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Romelu Lukaku

Hatimaye Romelu Lukaku amebebwa rasmi na Everton kwa kitita cha pauni milioni 28.

Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji mwenye miaka 21 aliyefunga mabao 16 akiwa Everton kwa mkopo msimu uliopita sasa atatumika pale Goodison Park kwa miaka mitano.

Bosi wa Everton Roberto Martinez amsemea: "Usajili huu sio tu muhimu kwa msimu huu, ni siku muhimu katika historia ya klabu."

Lukaku alijiunga Chelse akitokea Anderlecht kwa pauni milioni 18 mwezi August 2011 lakini aliichezea mechi 15 tu.

Baada ya kutia saini Lukaku amsema, "Nina miaka 21, ninahitaji kucheza kwenye Timu bora. Nataka kuwa mahali palipo nigusa kisahihi”

"Niliamua haraka sana nilitaka kurejea. Hapa ndipo ninapotakiwa kuwa” Aliongeza Romelu Menama Lukaku.