Kenya yakata rufaa ya marufuku ya CAF

Image caption Kenya imekata rufaa ya marufuku ya kocha Adel Amrouche

Kenya imekata rufaa ya marufuku ya mwaka mmoja iliyopewa kocha wa timu ya taifa Adel Amrouche na shirikisho la soka barani Afrika CAF.

Amrouche alipigwa marufuku hiyo baada ya kudaiwa kumtemea mate afisa msimamizi wa mechi baina ya Harambee Stars ya Kenya na Comoros mwezi Mei.

katibu wa Shirikisho la soka la Kenya FKF Michael Esakwa ameiambia BBC kuwa tayari wameshatuma ombi la kukata rufaa kwa shirikisho la CAF .

Image caption Kenya imekata rufaa ya marufuku ya kocha Adel Amrouche

"baada ya kuona video ya tukio hilo linalodaiwa kutokea baada ya mechi nina hakika kuwa hakuna aliyetemewa mate ''.

Sadfa ni kuwa kocha mkuu wa Comoros Amir Abdou amepuzilia mbali uwezekano wa tukio hilo akisema haiwezekani kuwa Amrouche alimtemea mate afisa huyo.

''Mimi mwenyewe nili kuwepo na pia nilitazama video na kwa hakika ninaunga mkono FKF maanake hii ilikuwa ni mechi ambayo tulishiriki.''

Ujumbe huo wa kocha Abdou ulimpiga jeki Esakwa ambaye anasema kuwa taarifa hiyo itakuwa kati ya habari watakazopendekeza kutumiwa katika rufaa hiyo.

Image caption Kenya imekata rufaa ya marufuku ya kocha Adel Amrouche

Kufuatia marufuku hiyo ya Amrouche, Kenyasasa inamtegemea Kocha mbadala James Nandwa kuiongoza Kenya katika mechi ya mkondo wa pili ya kufuzu kwa mechi ya kuwania kufuzu kwa dimba la mabingwa wa Afrika dhidi ya Lesotho.

Mechi hiyo itachezwa wikiendi hii mjini Nairobi.

Kenya ilishindwa katika mkondo wa kwanza kwa bao moja kwa nunge ugenini.