Tineja Mnigeria kupokonywa dhahabu

Image caption Tineja Mnigeria kupokonywa dhahabu leo

Tineja kutoka Nigeria mshindi wa nishani ya dhahabu ya unyanyuaji uzani Chika Amalaha, anatarajiwa kupokonywa medali yake ya dhahabu na kupigwa marufuku ya kushiriki mashindano yeyote leo.

Hii ni baada ya chembechembe za dawa zilizopigwa marufuku kupatikana katika vipimo vya pili vya damu yake hii leo.

Tineja huyo mwenye umri wa miaka 16 aliwatamausha wapinzani wake aliponyanyua kilo 196 na kunyakua nishani ya dhahabu ya kitengo cha wanawake wasiozidi kilo 53.

Shirikisho la michezo ya madola linakutana hii leo kutoa tangazo hilo.

Mnigeria huyo alikuwa amesimamishwa kwa muda kushiriki mashindano yeyote hadi vipimo vya pili vifanyiwe uchunguzi.

Bara la Afrika lilipigwa na butwaa wachunguzi walipotangaza kuwa damu yake ilipatikana na chembechembe za dawa za kuongeza nguvu mwilini zilizopigwa marufuku za amiloride na hydrochlorothiazide.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Chika anatarajiwa kupokonywa dhahabu leo

Mkurugenzi wa mashindano hayo Mike Hooper likuwa mwanariadha wa kwanza kupatikana na doa japo kutokea wakati huo wanariadha wengine wamepatikana kutumia madawa hayo.

Mwanaridha wa mbio za mita 400 kutoka Wales Rhys Williams mwengine wa mbio za mita 800m Gareth Warburton pia wamepatikana walitumia madawa hayo yaliyopigwa marufuku.

Mwanariadha huyo chipukizi wa Nigeria alishinda medali ya dhahabu Ijumaa iliyopita huku Dika Toua akiipatia Papua New Guinea medali yao ya kwanza ye fedha kwenye michezo hii ya Jumuiya ya madola mwaka huu.

Santoshi Matsa wa India aliipatia medali ya Shaba.

Lakini sasa kudhibitishwa kwa makosa hayo ya Amalaha inamaanisha kuwa sasa Papua New Guinea ndio mshindi wa dhahabu huku India ikijinyakulia nishani yake ya fedha.

Wanariadha wote hao wanakanusha kutumia dawa yoyote iliyopigwa marufuku huku wakiwa wanafahamu

Shirikisho la kupambana na madawa ya kututumua misuli limekuwa likijaribu kukomesha utumizi wa madawa hayo kwa kuwapiga marufuku wanariadha waliopatikana na hatia kwa kipindi cha miaka miwili.