Madola yamalizika kwa kishindo

Haki miliki ya picha Reuters

Mashindano ya Jumuiya ya Madola yamemaliza katika mji wa Glasgow nchini Scotland huku mji huo ukimiminiwa sifa kem kem na Mkurugenzi Mkuu wa Shirikisho la Mashindano ya Jumuiya ya Madola Mike Hooper kwa kuandaa mashindano hayo.

Baada ya siku 11 ya matukio mbali mbali ya michezo 17 hatimaye sherehe za ufungaji wa mashindano zilifanyika katika uwanja wa Hampden Park siku ya Jumapili usiku huku wenyeji wa mashindano hayo Scotland wakimaliza wakiwa nafasi ya nne kwa kunyakua medali za dhahabu 19.

Huku England ikiwa nafasi ya kwanza kwa mara ya kwanza tangu miaka 28 iliyopita kwa kunyakua medali 58 za dhahabu, Australia ya pili kwa kuwa na medali 49 za dhahabu na Canada ikishika nafasi ya tatu kwa medali 32 za dhahabu.