Webb kufunza umma kuhusu urefa

Image caption Kazi ya Howard Webb ni kuelezea uamuzi wa marefa kwa mashabiki

Siku moja tu tangu refarii mtajika Howard Webb kustaafu sasa imebainika kuwa itakuwa ni jukumu lake kuelezea mashabiki uamuzi wa marefarii.

Aidha refarii huyo mwenye umri wa miaka 43 ,aliiambia BBC kuwa kutokana na tajriba yake kuu katika uamuzi wa mechi kubwa muungano wa wapiga vipenga ulimkabidhi jukumu la kupambanua uamuzi ambao mara nyingi huzua utata.

''tumemaliza msimu ambao nimeshiriki asilimia kubwa ya mechi ngumu kwa hivyo jukumu langu itakuwa kuangazia uamuzi ambao labda haitakuwa imeeleweka na mashabiki.''

Webb alijiuzulu jumatano baada ya kuamua mechi kwa miaka 25 .

Kabla ya kustaafu Webb alikuwa muamuzi katika mechi 500 za ligi ya Premia ya Uingereza mbali na zile za kuwania ubingwa wa FA.

Hata hivyo kilele cha tajriba yake ilikuwa fainali ya kombe la dunia la mwaka wa 2010 iliyoandaliwa huko Afrika Kusini .

Refarii huyo mwenye umri wa miaka 43 alianza kazi hiyo mwaka wa 1989.

"najivunia tajriba niliyonayo na sasa nawashukuru wenzangu kwa kunichagua kuwahudumia katika kazi hii mpya ," alisema Webb.

Webb amewahi kuamua fainali ya kombe la mabingwa barani Ulaya fainali ya ligi kuu ya premia ya Uingereza.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Webb kuelezea uamuzi wa marefa kwa umma

Katika kombe la dunia lililokamilika majuzi huko Brazil, Webb alimua mechi ya kundi Cha baina ya Colombia na Ivory Coast,na ile ya mchujo baina ya Brazil na Chile.

Amewahi tuzwa na malkia wa Uingereza mwaka wa 2011na tuzo la MBE .

Tangu atangaze kujiuzulu maelfu ya mashabiki wake na watani wake wamekuwa wakituma jumbe za kumsuta kutweza na wengine kumshabikia .

Hata picha zimechapishwa zinazomkejeli kwa baadhi ya maamuzi yake haswa katika mechi za Manchester United ambayo anasemekana alikuwa akiwapendelea kuwapa muda zaidi ya ule uliopo na hata kuwa penalti ambazo zinatashwishi.